Kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC), kimetangaza marufuku ya mwaka mmoja ya kuagiza mbwa kutoka nchi 113 kwa kuhofia ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

Marufuku hiyo inahusisha mbwa wote ikiwa ni pamoja na wale wanaotumika kutoa msaada wa kifikra kwa wanaohitaji usaidizi wa wanyama hao na wale ambao wamekuwa katika nchi zenye hatari katika miezi sita iliyopita.

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo pamekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaomiliki mbwa katikati ya janga la Corona.

Aidha kituo cha CDC kimesema kuwa wamiliki wa mbwa hao wengi wao wana vyeti bandia vya kuthibitisha matibabu ya kichaa cha mbwa

CDC imesema ni muhimu kuhakikisha afya na usalama wa mbwa walioingizwa Marekani na kulinda afya ya umma, na kuzuia kuletwa tena kwa virusi mbalimbali vya ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

Marufuku hiyo inalenga nchi tofauti ikiwa ni pamoja na Kenya, Misri, Brazil na Urusi.

Rais Samia awatumbua DC, DED Morogoro
Diamond: Ukimzingua Ali Kiba nitakuzingua, tuna chetu