Serikali ya Marekani imeungana na Uingereza kupinga uhalali wa uchaguzi wa urais wa Burundi uliomalizika leo kwa madai kuwa haukufuata misingi ya uwazi na umekiuka katiba ya nchi hiyo.

Marekani imesema kuwa itapitia upya makubaliano ya ushirika kati yake na nchi hiyo na kuwawekea vikwazo vya visa maafisa wote wanaodaiwa kuhusika na uvunjifu wa amani na haki za binadamu.

Wananchi wa Burundi wamepiga kura kumchagua rais huku kukiwa na taharuki kubwa ya uvunjifu wa amani kufuatia uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Taarifa kutoka nchini humo zimeeleza kuwa uchaguzi huo uliosusiwa na vyama vikuu vya upinzani ulimalizima usiku huku milio ya risasi na milipuko ikisikika katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Inaelezwa kuwa watu wawili walipoteza maisha.

Serikali ya Burundi iliwatuhumu wapinzani kuwa chanzo cha kuanzisha vurugu na kuchochea uvinjifu wa amani.

Kwa mujibu wa BBC, serikali ya nchi hiyo iliwanyima vibali waangalizi Afrika katika dakika za mwisho kabla ya kuanza uchaguzi huo huku ikiwaruhusu waangalizi kutoka Afrika Mashariki iliyowaalika.

Kenyatta Awatoa Hofu Wakenya Kuhusu Ziara Ya Obama Na Ushoga
Chelsea Yanawa Mikono Usajili wa Pogba