Marekani imesema kuwa inaitazama Tanzania kama Taifa la Afrika Mashariki lenye hali nzuri ya utulivu, uimara na demokrasia.

Hayo yamesemwa leo na Balozi wa Marekani nchini, Dkt. Donald John Wright, alipokuwa Ikulu baada ya kumkabidhi Rais John Magufuli Hati ya Utambulisho.

“Marekani inaiona Tanzania kama nchi ambayo iko imara, na ya kidemokrasia katika Afrika Mashariki, chanzo cha uhusiano imara na Marekani,” amesema Balozi Wright.

Balozi Wright pia amewaelezea Watanzania kama watu wakarimu, akikumbuka miaka 33 iliyopita alipokuja nchini kwa ajili ya kutoa huduma ya kitabibu, akijitolea katika hospitali ya Save the Children.

“Nataka nikueleze tu kuwa nilitengeneza heshima nzuri kwa Watanzania, nilibaini watu wazuri, wakarimu, wacheshi na wanawachukulia watu wasiowafahamu kama sehemu ya familia yao,” Balozi Wright amesema.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, alisema kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Marekani ni mzuri.

Profesa Kabudi alitoa mifano ya fedha zinazotolewa na Serikali ya Marekani karibu kila mwaka kuunga mkono maendeleo ya Tanzania.

Rais Magufuli pia alipokea Hati ya Utambulisho ya Balozi wa Vietnam nchini, akiwa Ikulu, Dar es Salaam.

Magaidi wavamia gereza, wapambana vikali na walinzi

Mtoto mdukuzi sugu wa Twitter ashikishwa adabu, alimdukua Obama, Bill Gates

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 3, 2020
Magaidi wavamia gereza, wapambana vikali na walinzi