Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imesema kuwa inatafakari kuwaondoa takribani makomando wa Marekani wote kutoka Niger na kufunga vituo vya kupambana na ugaidi katika Bara la Afrika.

Maafisa wa Jeshi la Marekani (Pentagon) wameliambia gazeti la The New York Times kuwa vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyopo Cameroon, Kenya, Libya na Tunisia vitafungwa iwapo Waziri wa Ulinzi, Jim Mattis atapitisha mpango huo, lakini Marekani itaendelea kuwa na uwepo wa kikosi kikubwa cha jeshi lake Nigeria na Somalia.

Kwa mujibu wa The Times, hatua hiyo ni sehemu ya kubadilika kwa mkakati wa Marekani kutoka kupambana na vikundi vya waasi na kuangalia masuala makubwa.

Aidha, Jambo hilo limeibuka baada ya shambulizi dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Niger mwaka 2017 ambalo liliwauwa wanajeshi wa Marekani wanne, ambapo Pentagon ilikiri kuwa kulikuwa na udhaifu upande wao.

Hata hivyo Jenerali Thomas Waldhauser, mkuu wa kikosi maalum cha Marekani Afrika, African Command, siku za hivi karibuni amesema kuwa Marekani haitajiondoa katika kupambana na ugaidi Afrika.

 

 

Jose Pekerman aibwaga Colombia
Video: Pigo la mwisho kwa Makonda, JPM afurahia kichaa cha Waziri Mpina, Dkt. Bashiru usiyemjua