Idadi ya vifo nchini Marekani yongezeka na kufikia 4,491 ndani ya saa 24 kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha John Hopkins.
Hata hivyo, vifo hivyo vinaweza kuwa vinajumuisha watu waliofariki wakihusishwa kuwa na COVID19 na Madaktari kujiridhisha hivyo lakini bila mgonjwa kupimwa maabara.
Aidha Marekani ilikuwa ikitangaza idadi ya vifo vya wagonjwa waliopimwa maabara na kuthibitika kuwa na Ugonjwa huu.
Mpaka kufikia jana Chuo hicho kimetoa takwimu za kidunia kuhusiana na mwenendo wa ugonjwa wa COVID 19 vifo vikiwa ni 137,078 huku jumla ya visa vilivyothibitishwa kufikia takribani milioni mbili.