Waziri wa Mambo Ndani wa Marekani, James Mattis amesema kuwa tishio lolote kutoka Korea Kaskazini kwa Marekani ama washirika wake litajibiwa vikali na jeshi la nchi hiyo ambalo limejiandaa kwa kuitwanga nchi hiyo.
Aidha, Rais Trump ameonya kuwa Marekani inaweza kusimamisha kufanya biashara na nchi yoyote inayoshirikiana kibiashara na Korea Kaskazini kwa kuwa nchi hiyo tayari ilishawekewa vikwazo.
Nchi ya China ndio mshirika mkuu wa biashara wa Korea Kaskazini ambapo amesema kuwa nchi hiyo imekuwa tishio kwa usalama wa dunia kitu ambacho kimesababisha kuwekewa vikwazo.
Hata hivyo, kwa upande wake Korea Kusini imesema kuwa imefanya majaribio matano kama majibu ya jaribio la nyuklia la Korea Kaskazini ambayo imekuwa ikifanya majaribio hayo mara kwa mara.
-
Jiwe kubwa tishio kwa Dunia, wanasayansi wahaha
-
Trump apanga kuwaelewesha Korea Kaskazini kwa kitu kimoja tu