Ubalozi wa Marekani nchini umewatahadharisha raia wa Marekani walioko nchini kuhusu mpango wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya maandamano nchi nzima kupitia oparesheni waliyoipa jina la UKUTA, Septemba 1.

Taarifa ya Ubalozi huo iliyowekwa pia kwenye mtandao wa kidiplomasia wa Osac, imewataka raia wa Marekani kuchukua tahadhari iwezekanavyo kujiepusha na maeneo ambayo maandamano hayo yanaweza kupitia.

“Ingawa maandamano yamepangwa kuwa ya amani yanaweza kubadili na kuwa vurugu. Jihadharini na maeneo ambayo maandamano yatafanyika na chukueni tahadhari katika maeneo ya mikusanyiko na maandamano,” imesema sehemu ya taarif hiyo.

Hata hivyo, tayari juhudi za kusaka suluhu kati ya upande wa Serikali na Chadema zimeanza juzi kwa kuwakutanisha viongozi wa dini, viongozi wa CCM pamoja na muwakilishi wa Serikali.

Waziri wa Fedha Aigomea Polisi Nchini Afrika Kusini
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Atoa Neno Kuhusu Mamilioni Ya Raisi Magufuli