Marekani imewafukuza Wanadiplomasia 60 wa Urusi wanaotuhumiwa kujihusisha na ujasusi kuondoka mara moja nchini humo.
Hatua hiyo ya Marekani, imeungwa mkono na Ufaransa, Ujerumani na Poland, ambapo nchi hizo zimesema kuwa hatua hiyo ni kujibu kwa pamoja shambulizi la sumu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi na binti yake huko mji wa Salisbury, Uingereza.
“Marekani imechukua hatua hii kwa kushirikiana na washirika wetu wa NATO na nchi nyingine duniani kujibu shambulizi lililofanywa na Urusi wakitumia sumu katika ardhi ya Uingereza, ikiwa ni mwendelezo wa mbinu za kudhoofisha shughuli mbalimbali duniani,” amesema msemaji wa White House Sarah Huckabee Sanders.
Hata hivyo, Ujerumani na Poland wamesema kuwa wameamrisha wanadiplomasia wanne wa Urusi kuondoka katika nchi hizo, wakati huko Lithuania, wanadiplomasia watatu wameamrishwa kuondoka nchini.