Maafisa wa Idara ya Ujasusi ya Marekani, wamesema Urusi na Iran zimetumia taarifa za wapiga kura, ili kuwatisha raia wa Kimarekani pamoja na kujaribu kuwafanya wapoteze imani na mfumo wa uchaguzi.

Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi Marekani John Ratcliffe, amesema Oktoba 21, Urusi na Iran zilijaribu kuingilia kati uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika Novemba 3, kwa lengo la kushawishi maoni ya wapiga kura.

Katika mkutano na waandishi habari, Ratcliffe amesema Iran na Urusi zimeweza kupata baadhi ya taarifa za usajili wa wapiga kura na kuzitumia kusambaza taarifa za uwongo kwa wapiga kura waliojiandikisha ili kuhujumu demokrasia ya nchi hiyo.

Ratcliffe ameongeza kwamba maafisa wa serikali tayari walishagundua kwamba Iran imetuma barua pepe zinazolenga kuwatisha wapiga kura, kuchochea machafuko katika jamii na kuchafua jina la Rais Donald Trump.

Ligi Kuu Tanzania Bara: KMC FC yatangulia Mwanza
Young Africans Vs Polisi Tanzania, Tanzania Prisons Vs Simba SC