Kufuatia Benki Kuu ya Tanzania, kuendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuongeza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika kufanya miamala, Serikali inapendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, 2015, ili kufuta tozo kwa siku kwa kila laini ya simu.

“Napendekeza kufuta tozo kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio kwa
watumiaji ili kuchochea matumizi ya kielektroniki katika miamala mbalimbali.”

Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba, ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati wakati akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2023/2024.

Amesema, “hatua hizo ni pamoja na usasishaji wa Mifumo ya Malipo ya Taifa (upgrading), ikiwemo kukamilika na kuanza kutumika kwa Mfumo wa Malipo wa papo kwa papo (Tanzania Instant Payment System – TIPS), na usimamizi thabiti wa mifumo ya malipo nchini.”

Aidha, Dkt. Mwigulu amesema, uboreshaji wa miundombinu hiyo ni hatua muhimu ya kufikia malengo ya ujumuishwaji wa wananchi wengi kwenye mfumo rasmi wa fedha na pia kwa nchi kuelekea kwenye uchumi wa kidijitali.

Serikali yapendekeza ufutaji ada Vyuo vya Ufundi
Nafuu gharama za umilikishaji Ardhi wapiga hodi