Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi imeridhia muenendo wa Taifa unaofanya na Mwenyekiti wa Chama Rais Samia Suluhu Hassan juu ya maridhiano na mapatano na Chama pinzani ili kuleta amani ya taifa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Shaka Hamdu Shaka akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za makao maku ya CCM jijini Dodoma, amesema kuwa Kamati hiyo ilikaa kikao ikapokea taarifa kuhusiana na Masuala yanayoendelezwa na Mwenyekiti wa CCM na kupitisha taratibu zote za mashauriano, mapatano na ushirikiano.
Amesema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ilikutana Mei 22, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma.
“Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imepokea na kujadili masuala na taarifa ya mambo ya kitaifa ikiwemo ambayo amekua akiyafanya Rais Samia katika kujenga maridhiano ya kisiasa nchini na kwa Watanzania kwa Ujumla. Kamati Kuu imeridhia na kumpongeza Kiongozi wetu katika hatua zote anazochukua katika kuzingatia na kuendeleza urithi ulioachwa na waasisi wa Taifa Letu,” amesema Shaka
“Tumeona ambavyo Mheshimiwa Raisi amekuwa akikutana na viongozi wa vyama tofauti vay upinzani ikiwemo chama kikuu cha Upinzani CHADEMA, na yote ni katika nia ya kuimarisha mapatano na kuwaunganisha watanzania, na kusimamia maridhiano ya kisiasa ambayo yataleta mustakabali mwema wa Nchi yetu na hatimae amani italayoleta maendeleo,” amesema Shaka.
Ameongeza kuwa kutokana na katiba na Ilani ya CCM inavyotaka katika kulinda haki za wananchi za kikatiba ni lazima kiła unapozungumzia utawala wa kidemokrasia, maisha ya uhuru na Haki, na mienendo ya kukukubali maoni ya wananchi kuwepo na maridhiano ya mabaraza ya Chama vya siasa.
“Chama Cha Mapinduzi kimetambua mazingira na mahitaji ya kisiasa kwenye jamii kwa sasa, hivyo chama kimeona ni dhamira ya dhati ya kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika juhudi za kuendeleza demokrasia nchini.” Ameongeza Shaka.
Shaka amesema kuna dhamira njema za viongozi wa vyama vya siasa pamoja na Rais Samia katika mikutano iliyopita na itakayotokea na yote ni kuendelea kusubiri na kuvumilia kuona matokeo ya mikutano hiyo.
Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi amekua akifanya mikutani na viongozi wa Chama vya siasa ikiwemo Ndugu Freeman Mbowe wa CHADEMA ambaye alionana nae alipotoka Gerezani, Ndugu James Mbatia wa NCCR Mageuzi, na Ndugu Ibrahim Lipumba wa CUF.