Mshambuliaji wa klabu ya Nice ya nchini Ufaransa Super Mario Balotelli amemuunga mkono Luis Suarez katika harakati za kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2016.

Balotelli ambaye kwa sasa anaonekana kupevuka kiakili kutokana na mabadiliko ya soka lake analocheza katika ligi ya nchini Ufaransa, amesema mshambuliaji huyo kutoka nchini Uruguay ana vigezo vyote vya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo ambayo kilele chache kitakuwa mwezi Januari mwaka 2017.

Amesema uwepo wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2016, haimaanishi kama ubora wa Luis Suarez unapotezwa, zaidi ya kuongeza upinzani.

Messi na Ronaldo wamekua wakichuana katika tuzo hiyo tangu mwaka 2008, jambo ambalo Balotelli anaamini imetosha kwa kipindi hiki, na anaamini umewadia wakati kwa watu wengine kama Suarez kupewa heshima yake.

Hata hivyo Balotelli ametoa mfano ambao umempa msukumo wa kuamini Suarez anapaswa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa kusema, hatua ya kutwaa kiatu cha dhahabu kama ishara ya mfungaji bora katika ligi za barani Ulaya kwa msimu uliopita inatosha kwa kila mtu kuamini, mshambuliaji huyo anastahili heshima.

Kwa msimu uliopita Suarez alifunga mabao 40 akiwa na klabu yake ya FC Barcelona ambayo ilitwaa ubingwa wa ligi ya nchini Hispania.

Video: Ifahamu siri ya wasanii wa Bongo kukosa tuzo za MTV MAMAs 2016, walichofanya
Video: Simba tumepata pigo kubwa sana - Rage