Uongozi wa klabu ya Borussia Dortmund, umeanza kufanya mazungumzo na mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, kwa ajili ya kumsajili kiungo Mario Gotze.

Borussia Dortmund, wamedhamiria kumrejesha Westfalenstadion kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, baada ya kuonyesha nia ya kusalia nchini Ujerumani ambapo amepazoea.

Aliyewahi kuwa meneja wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp ambaye kwa sasa yupo nchini England akikinoa kikosi cha Liverpool, alikua akitoa msukumo wa kutaka Gotze asajiliwe huko Anfield, baada ya kusikia hatokuwepo Allianz Arena kwa msimu ujao.

Mtendaji mkuu wa FC Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge, amethibitisha kuanza kwa mazungumzo ya usajili wa Gotze na amesisitiza kuwa na uhakika wa kufikia muafaka.

“Tumeanza kufanya mazungumzo na Borussia Dortmund na kuna dalili zimeanza kuonekana kuhusu mustakabali wa jambo hilo, nina imani tutafikia pazuri kwa kumaliza mpango uliowekwa.” Alisema Karl-Heinz Rummenigge alipozungumza na Sport1.

Gotze amewahi kutwaa ubingwa wa ligi ya nchini Ujerumani mara mbili, akiwa na klabu ya Dortmund kabla ya kujiunga na Bayern mwaka 2013, lakini ameshindwa kujihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza  tangu alipowasili mjini Munich, misimu mitatu iliyopita.

Zembwela Akerwa naMabinti Wanaoweka Picha za Utupu Mitandaoni
Majaliwa Asisitizia Suala la Maji Safi na Salama Afrika