Bingwa wa michuano ya tennis ya Wimbledon mwaka 2013, Marion Bartoli, ametengua uamuzi wake wa kustaafu na kutangaza rasmi kurejea katika mchezo huo kuanzia msimu ujao wa mashindano.
Marion alikumbwa na matatizo ya kiafya yaliyosababisha kustaafu kwake na katika kauli yake ya mwisho mwaka 2016 alisema anahofia uhai wake baada ya kugundulika kuwa na vijidudu ambavyo havijafahamika chanzo chake mpaka leo.
Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 33, baada ya kutangaza kustaafu mchezo huo Agosti 14 mwaka 2013, amekuwa akifanya kazi mbalimbali ikiwemo ya uchambuzi wa mchezo wa tennis.
Marion ataanza kuonekana dimbani mwezi Machi mwakani wakati wa mashindano ya Miami Open.