Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, limteua muamuzi kutoka nchini England, Mark Clattenburg kuwa msimamizi wa dakika 90 za mchezo wa hatua ya fainali utakaoshuhudia Ureno wakipambana na Ufaransa mwishoni mwa juma hili.

UEFA, wamemtangaza muamuzi huyo, kwa kuzingatia uwezo na umakini wake anapokua katika kazi yake ya uchezeshaji kwa kuzingatia sheria 17 za mchezo wa soka kwa kutenda haki, tena kwa wakati.

Kwa mwaka huu, huenda ikawa heshima kubwa kwa Clattenburg, kufuatia uteuzi wake ambao umekua ukiangukia katika michezo muhimu ya hatua ya fainali ambayo imekua ikimaliza salama wa salmini.

Clattenburg aliteuliwa kuchezesha mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid na ule ya kombe la FA kati ya Manchester United dhidi ya Crystal Palace.

Mchezo wa fainali ya Euro 2016, umepangwa kufanyika Julai 10 katika uwanja wa Stade de France mjini Paris.

Waziri Mkuu Asitisha Vibali Vya Uvunaji Mbao
Mgombea Urais wa Democrat, Hillary Clinton aanza kuchunguzwa