Mkurugenzi mtandaji wa klabu bingwa nchini Italia Juventus,  Beppe Marotta amemponda kiungo wa klabu ya New York City FC ya nchini Marekani, Andrea Pirlo kwa kumtaka atangaze kustaafu kuitumikia timu ya taifa.

Marrota ameshindwa kujizuia na kuanika hadharani hatua ya kumponda kiungo huyo ambaye alikuwa mchezaji wa Juventus kwa miaka miwili iliyopita, baada ya kushuhudia mchezo wa kuwania kufuzu fainali za barani Ulaya mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Pirlo alikua miongoni mwa kikosi cha Italia kilichopambana dhidi ya timu ya taifa ya Malta na kuibuka na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Kiongozi huyo wa Juventus amesema ni wakati mzuri kwa Pirlo mwenye umri wa maika 36 kufikiria kufanya maamuzi ya kuwaachia vijana ili waendelee kuitetea Italia.

Marotta, aliendelea kubainisha kwamba ni aibu kubwa kwa timu yao ya taifa kuendelea na mtu mwenye umri mkubwa ili hali kuna vijana wengi ambao wanaweza kuchukua nafasi yake na wakafanya vyema.

Hata hivyo imedaiwa kwamba Marotta aliyasema maneno hayo kwa kwa kumshambulia Pirlo, kutokana na kutokua na maelewano mazuri na mchezaji huyo kufuatia tofauti zilizojitokeza mwishoni mwa msimu uliopita.

Pirlo aliamua kuikacha Juventua FC na kwenda kusaka mahala pengine pa kucheza soka lake, baada ya kufunguliwa mlango wa kuondoka Juventus Stadium ili hali bado alikua tayari kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Mtu anayetajwa kusababisha safari ya Pirlo kuondoka nchini Italia na kwenda nchini Marekani kusaka mahala pa kuendeleza soka lake ni Marotta ambaye alikua kishawishi kikubwa kwenye uongozi kwa kutaka mchezaji huyo asipewe mkataba mpya.

Karatu Yamwaga Dk Slaa
Unavyopaswa Kujibu Unapotakiwa Kuelezea Udhaifu Wako Kwenye Usaili Wa Kazi