Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus, wamesema kiungo Paul Pogba alikua na thamani ya Euro million 100 wakati wa usajili wa majira ya kiangazi ambao ulifungwa rasmi siku ya jumanne jioni.

Mtendaji mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta amesema kutokana na thamani ya kiungo huyo ilikua vigumu kwa klabu zilizokua zimewasilisha ofa kwa ajili ya kumsajili kutimiza lengo la kumuhamisha kutoka Juventus Stadium.

Marotta amesema mara kadhaa walikua na mikutano na viongozi wa klabu hizo ambazo zilionyesha nia ya kumsajili Pogba, lakini msimamo wao wa kutotaka kumuuza chini ya thamani yake.

Kutokana na mpango huo kushindikana Marrota amesisitiza jambo la kufurahishwa na kuendelea kubaki na Paul Pogba katika msimu huu, ambao wamedhamiria kufanya makubwa zaidi ya misimu kadhaa iliyopita.

Pogba mwenye umri wa miaka 22 alikua kwenye rada za klabu za Man utd, Chelsea, Real Madrid pamoja na FC Barcelona.

Katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi Juventus walikubali kuwaachia baadhi ya wachezaji wao kama Andrea Pirlo, Arturo Vidal pamoja na Carlos Tevez.

Wakati huo huo Marotta amesema wamesikitishwa na hatua ya kushindwa kumsajili kiungo Julian Draxler ambaye amejiunga na klabu ya VFL Wolfsburg akitokea Schalke 04.

Amesema walikua wamefikia pazuri juu ya kumsajili kiungo huyo, lakini kuingia kwa VFL Wolfsburg kuliharibu taratibu zao na hatimae walikubali kuacha dili hilo kuendelea kujadiliwa na viongozi wa klabu za nchini Ujerumani ambazo zilikubaliana kufanya biashara zenyewe kwa zenyewe.

Magufuli: Mimi Ni Maji Moto Kuunguza Mafisadi
Zlatan: Nipo Tayari Kwa Lolote