Klabu ya Manchester United bado inasisitiza kutomuuza kiungo wake kutoka nchini Ubelgiji, Marouane Fellaini.

Taarifa hizi zinakuja baada ya kuendelea kuwepo kwa tetesi zinazoihusisha klabu ya AC Milan kutaka kumchukua kwa mkopo kiungo huyo.

Mtandao wa klabu ya Manchester United umenukuu kauli ya bosi wa Mashetani hao, Louis Van Gaal akisisitiza kuwa hawana sababu ya kumuuza kiungo huyo kwa dau lolote.

“Kuna taarifa zinazozagaa mitandaoni kuhusiana na Fellaini kutaka kununuliwa ama kutolewa kwa mkopo, katu si taarifa za kweli kwasababu klabu hii kwa sasa haina azma hiyo.”

“Ninachotaka kusema hata sasa ni kwamba, Fellaini bado ana majukumu akiwa hapa na kwamba nimezugumza nae na kuniambia bado anahitaji kubaki hapa kwa miaka mingi ijayo,” alisisitiza Van Gaal na kuongeza.

“Wakati mwingine taarifa kama hizi zinaweza kumchanganya mchezaji, lakini nimefanya uamuzi wa busara kumwita na kuzungumza nae juu ya mustakabari wake Old Trafford.”

“Kila kitu kipo sawa juu ya Fellaini kubaki United. Nimemthibitishia kuwa hata klabu ina imani nae na amejisikia faraja katika hili, hivyo ninatamka wazi kuwa hatouzwa kwa dau lolote wala kutolewa kwa mkopo.”

Fellaini alitua Old Trafford kwa kitita cha pauni mil. 27.5 akitokea Everton mnamo mwezi Agosti, 2013, lakini anajikuta hana msimu mzuri chini ya Van Gaal.

Van Gaal amempanga kiungo huyo katika michezo minne ya Ligi ya premier, ambapo kwa sasa yupo katika kampeni ya kuendelea kumshawishi Mholanzi huyo ili kuweza kupatanamba ya kudumu kikosini.

Boateng Azungumza Kwa Mara Ya Kwanza Akiwa AC Milan
Ronald Koeman: Wanyama Ataendelea Kuwa Mali Ya Southampton