Manchester United iko tayari kuongeza mkataba wa Aaron Wan-Bissaka na Victor Lindelof, vyanzo vimeiambia ESPN, lakini mabosi wa klabu hiyo wamejipa muda kabla ya kufanya uamuzi juu ya hatima ya Anthony Martial.
Mfaransa huyo, ambaye ana mkataba hadi mwisho wa msimu pamoja na chaguo la kuongeza mwaka mmoja, alikumbwa na majeruhi msimu uliopita ambapo alianza mechi 11 pekee za Ligi Kuu England.
Kwa sasa amepoteza namba kwa mchezaji aliyesajiliwa majira ya joto, Rasmus Hojlund kwa kiwango kikubwa msimu huu, aliyefunga bao moja katika mechi tisa, na hali yake Old Trafford ni ngumu kwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi.
Chanzo kimoja kiliiambia ESPN, United walikuwa tayari kumwacha Martial aondoke msimu wa joto, lakini ofa pekee ya kweli iliyopokelewa ilitoka Ligi Kuu ya Saudia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikataa nafasi ya kuingia kwenye mazungumzo juu ya kuhama.
United wameweka wazi chaguo lao kwa Martial, kutegemeana na jinsi atakavyocheza kati ya sasa na mwisho wa msimu.
United, hata hivyo, wanatazamiwa kuchukua mtazamo tofauti kwa walinzi Wan-Bissaka na Lindelöf.
Wan-Bissaka ameshinda tena nafasi yake katika timu ya Erik ten Hag baada ya mwanzo mgumu chini ya Mholanzi huyo.
Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini United wana fursa ya kuuongeza kwa mwaka mmoja zaidi hadi 2025.
Klabu hiyo imepanga kutekeleza chaguo hilo kabla ya mwisho wa mwaka huku pia ikifungua mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu.
United wako katika hali sawa kwa Lindelöf, ambaye ana mkataba hadi majira ya joto pamoja na chaguo la kuongeza mwaka mmoja.
Mchezaji huyo wa wa Sweden amefanya vya kutosha kumshawishi Ten Hag kuwa ana hatima ya kuishi Old Trafford na klabu iko tayari kuamsha nyongeza yake hadi 2025.