Baada ya kushiriki kukipigia debe Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu uliokamilika baada ya Dkt. John Magufuli kuwa rais wa Tanzania huku chama hicho kikizoa viti vingi Bungeni, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja Mkandamizaji ameamua kuwania nafasi ya ubunge wa Ludewa.

Msanii huyo wa sanaa ya vichekesho ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za injili, ametangaza rasmi kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Ludewa ambalo uchaguzi wake uliahirishwa baada ya mgombea aliyekuwa akitetea nafasi ya ubunge wa jimbo hilo, Deo Filikunjombe kufariki kwa ajali ya ndege wakati wa kampeni.

Masanja ameingia kwenye chujio la kura za maoni za CCM kumpata mgombea mmoja atakayechuana na wagombea wa vyama vya upinzani. Masanja atachuana na wagombea wengine nane kwenye kura za maoni ikiwa ni pamoja na mdogo wa marehemu Deo Filikunjombe anayeitwa Philipo Filikunjombe.

CCM Tanga Wavurugana, Waahidi Kufanya Maandamano
Mahakama Yazima Neema Ya Nyongeza ya Mishahara ya Walimu Kenya