Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino wa Ruvu Shooting Masau Bwire, amekiri timu yao ipo katika hali ngumu, baada ya kukubali kufungwa na Azam FC mwishoni mwa juma lililopita.

Ruvu Shooting ilipoteza mchezo huo Jumamosi (April 22) kwa kufungwa 3-1, ikiwa nyumbani katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro hali ambayo imeifanya timu hiyo kuendelea kuburuza mkia wa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Masau Bwire amesema timu yao bado ina nafasi kubwa ya kusalia Ligi Kuu, lakini inapaswa kupambana vilivyo katika michezo iliyosalia ili kupata alama zitakazowaokoa.

“Tunacheza mchezo mgumu mgumu na tunapita kwenye nyakati ngumu hivyo tunapambana katika hali hii ili kupata matokeo mazuri.”

“Ninaamini nafasi bado ipo na tunaweza kufanya jambo katika michezo iliyosalia, lakini nikiri tu hali tuliyonayo kwa sasa sio nzuri kabisa.” Amesema Masau Bwire

Ruvu Shooting wanashikilia nafasi ya 16 wakiwa na alama 20 baada ya kucheza michezo 27 jambo linaloonyesha hatari kwao ikiwa watapoteza michezo mitatu ilizobaki wanaweza kushuka daraja.

Ithibati kitabu cha Muungano imekamilika - Jafo
Heche amuhamisha Wizara Mwigulu Nchemba