Kufuatia kauli iliyotolewa jana (Desemba 02) na Mkuu wa Idara ya Habari na Masiliano ya Simba SC Haji Manara kuweka hadharani mpango wa kutowaruhusu mashabiki wa Young Africans kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa watakapocheza dhidi ya Plateau United, msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire, ameonesha kuchukizwa na kauli hiyo.

Masau Bwire amendika makala fupi na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii, kwa kuamini ni njia sahihi ya kumfikishia ujumbe Manara, kufuatia kauli yake aliyoitoa kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatano.

“Mpira wa miguu, usitugawe Watanzania

Mpira wa miguu, chimbuko lake hasa, ulilenga kuburudisha watu, kuwaleta pamoja, kuimarisha amani, umoja na mshikamano, katika hilo, nadhani sote ni mashahidi.

Raha ya mpira wa miguu ni kuzodoana, nikimaanisha, uwepo upinzani, ushangilie unaposhindwa na uzomewe na mpinzani wako unapofungwa, huo ndio mpira wa miguu, na ndiyo maana yake, tena, ndiyo raha ya soka.

Yeyote atakaecheza na yeyote, yeyote aliruhusiwa kuingia kushangilia na kumzomea yeyote kwa mapenzi na kujisikia kwake,  hii ndiyo maana ya ushindani na upinzani, popote Duniani,  katika ulimwengu wa soka, ndivyo ilivyo, watu wa mpira, wenye kujua kusudi lake hasa, ndivyo wafanyavyo, hawabaguani, wala kuhoji nani kaingia uwanjani kumshangilia au kumzomea nani, kila mmoja na mapenzi yake!

Hapa kwetu nionavyo,  kama haitafanyika makusudi ya kurekebisha na kuzuia yanayoendelea,  mpira wetu wa miguu, utatugawa Watanzania,  utatuondolea umoja kati yetu, utatuletea huasama, vurugu na amani kutoweka,  badara ya burudani,  soka letu litageuka vita, maumivu na hata kuuana!

Kwa nini tufike huko, kwa faida ya nani, na kwa lipi?

Tafakari……

Masau Kuliga Bwire – Mzalendo.

KMC FC waisuburu kwa hamu Dodoma Jiji
UN yaiondoa bangi kwenye orodha ya madawa hatari ya kulevya