Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali dhidi ya Mkandarasi ambaye ametelekeza ujenzi wa mradi wa Umwagiliaji kwenye Gereza la Kilimo Idete mkoani Morogoro.

Ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea gereza hilo kwaajili ya kujionea mradi huo ambapo alielezwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Ramadhan Nyamka.

Aidha, baada ya kupata maelezo ya mradi huo, Masauni amelitaka Jeshi la Magereza kufanya uchunguzi dhidi ya Mkandarasi huyo na ikithibitika anamakosa akamatwe na achukuliwe hatua za kisheria.

Hata hivyo, Mkandarasi huyo ametelekeza mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 2.5 tangu mwaka 2016 kitu ambacho kimemfanya Waziri Masauni atoe agizo hilo akisisitiza kumchunguza na kumchukulia hatua za kisheria endapo itathibitika Mkandarasi ana makosa

Nape awataka vijana kuchukua maamuzi magumu
Spika wa Bunge ajiuzulu akipinga vitendo vya Serikali