Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuna haja ya kuwekwa mfumo mzuri wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi, ili kutekeleza sera ya Polisi Jamii kwa lengo la kufanikisha uondoaji wa matukio ya uhalifu Nchini.

Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Bububu Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi, amesema mbali na uwepo wa mafanikio katika usimamizi wa ulinzi na usalama, bado zipo changamoto baina za utekelezaji wa ulinzi shirikishi kwa pande hizo mbili.

Awali, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamad Khamis Hamad amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuchukuwa hatua mbalimbali za kutatua changamoto katika utekelezaji ulinzi shirikishi, ikiwa ni pamoja na kujenga uwelewa kwa Askari na wananchi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bububu, Mwantakaje Haji Juma amewahimiza wananchi kushirikiana na Taasisi za haki Jinai katika kufuatilia kesi zao na kutoa ushahidi, ili zipate mafanikio Mahakamani huku Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Suzan Kunambi akiwasihi wananchi kuacha tabia ya usuluhishi wa kesi mitaani.

Dkt. Mwinyi agusia fursa uwezeshaji Wananchi kiuchumi, ajira
Uwekezaji: Waziri Mkuu ayapigia chapuo Makao makuu