Mwanamuziki kutoka Nairobi Kenya Mohammed Ali Said maarufu Masauti, ametoa kauli yake kuhusu sakata lililotokea kwenye tamasha la Mbosso mjini Mombasa baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa alishushwa jukwaani wakati akitumbuiza kwa sababu zisizojulika.
“Sijataka kuongelea issue ya show ya Mombasa lakini pia nimeona nivunje ukimya ili kuepuka unafiki. Najua mashabiki zangu wana hofu kutaka kujua what exactly happened ndio nisingependelea mtu atumie jina langu kuelezea my side of the story.
Nataka niwaombe tu kwanza tukio hili lililotokea lisitumike kumharibia rafiki yangu Mbosso jina wakati siye aliyeandaa show hii,” amesema Masauti.
Mwimbaji huyo aliendelea kutoa maelezo ya kuhusu mwanadada ambaye alizua sintofahamu kwenye tamasha hilo, hali iliyomlazimu mtangazaji maarufu wa nchini Kenya William Tuva kuingilia kati kabla ya yeye ‘Masauti’ kumaliza muda wake jukwaani.
“Makosa yatupiwe waandaaji wa show hiyo mchwara tena sio wote ni dada mmoja tu ambaye nisingependa nimtaje jina, Yeye ndio hakutaka kuheshimu kazi yangu na kunionyesha thamani kama msanii wa nyumbani.
Lakini kama mpambanaji niliamua kuweka kazi kwanza maana sipendi kuweka hisia zangu mbele kwakua nina familia nyuma inayoniangalia mimi tu.
Siku ile ya show walienda kinyume na mahitaji yangu lakini wala sikuvunjika moyo kwakua ni kijana ninayepambania sanaa yangu ili familia yangu ipate rizki, Hakukua hata na usafiri kwa ajili yangu ili kufika kwenye sound check,” aliongeza masauti.
Nyota huyo mmiliki wa hit song ‘No stress’ pia aligusia swala la promota wa show hiyo kutosimamia ipasavyo matakwa ya makubaliano yao ya awali ikiwa ni pamoja na maswala ya kiusafiri nk.
“Baada ya kama nusu saa hivi, nikiendelea kuperform nikaona nyuma kuna mvutano unaendelea kati ya management yangu na watu kwenye stage.
Yule yule dada alitaka nikatize show katikati Vita hiyo iliendelea kati yao na uongozi wangu ambao ulipinga hilo wazo lao la kusimamisha show katikati.
Dj alisimamisha show kwasababu yule dada alimtishia kutomlipa, mvutano uliendelea akaja willy Tuva aliyeingilia kati na kukataa mziki ukatishwe namna hio.
Aliungana nasi show ikaendelea. Nikaimba na mashabiki zangu hadi wakati wangu ukaisha ndo nikashuka kwenye stage,” aliezea Masauti