Serikali mkoani Iringa imesema hakuna njaa kwa sababu msimu wa mwaka 2015/2016 walizalisha tani zaidi ya milioni 1.4 zikijumuisha mazao ya nafaka, mizizi na mazao jamii ya kunde.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza,alipokuwa akiongea kuhusu upatikanaji wa chakula, amesema kuwa baadhi ya wananchi wengi wamejawa na tamaa ndiyo maana wanauza chakula badala ya kuhifadhi kwa ajili ya matumizi ya familia zao.
“Kila kaya inatakiwa kuhakikisha ina chakula cha kutosha badala ya kukiuza, na wataalam wa chakula wataendelea kupita kila nyumba kuhimiza utuinzaji wa chakula sambamba na uwiano wa mahitaji halisi,” amesema Masenza.
Aidha, amesema kwa sasa Mkoa huo una ziada ya mazao ya nafaka tani 756,369.92 na kunde tani 61,584.63.
Hata hivyo ametoa wito kwa baadhi ya wananchi kuthamini familia zao kwa kuhifadhi chakula badala ya kukiuza kwa tama zao za kupata fedha kirahisi.