Shirikisho la Soka Barani Afrika *CAF* limeiruhusu timu ya Simba kuingiza washabiki 10,000 katika mchezo wa mzunguuko watano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, utakaochezwa Jumamosi (April 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dares salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Shirikisho la soka nchini Tanzania *TFF*, CAF imeafiki mabingwa hao wa Tanzania Bara kucheza na mashabiki 10,000 baada ya kuzuia mashabiki kwenye mchezo wa mzunguuko wanne dhidi ya Al Merrikh uliochezwa mwezi Machi Uwanja wa BenjaminMkapa.

Uongozi wa Simba SC kupitia kwa mwenyekiti wake Multaza Mangungu ulitoa taarifa za kuwasilisha ombi CAF la kutaka mashabiki wao kurejeshwa Uwanjani, kwenye mchezo dhidi ya AS Vita ambao mandaalizi yake yanaendelea kufanywa jijini Dar es salaam.

Kuruhusiwa kwa mashabiki 10,000 huenda ikwa ni sehemu ya majibu ya Simba SC waliowasilisha CAF, kama ilivyokuwa imeelezwa na Multaza Magungu alipozungumza na waandishi wa habari Jumapili (Machi 28), baada ya mchezo wa Tanzania dhidi ya Libya.

Tayari AS Vita wameshaanza safari ya kuja nchini kwa ajili ya mchezo huo, ambao umepangwa kuchezwa mishale ya saa kumi jioni, kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba SC inaongoza msimamo wa Kundi A kwa kufikisha alama 10, ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama 7, AS Vita inashika nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 4 na AlMerrikh wanaburuza mkia kwa kupata alama moja kwenye michezo minne waliocheza.

Miquissone, Kagere kutinga kambini leo
AS Vita Club kuwasili na wachezaji 24, Djuma Shabani aachwa