Mashabiki wa Manchester United wamepatwa na hasira baada ya kusikia ripoti zinazodai kwamba winga wao Facundo Pellistri huenda akatolewa kwa mkopo kabla ya dirisha hili kufungwa.

Winga huyo wa kimataifa wa Uruguay anajiandaa kwenda kujiunga na Sheffield United kwa muda.

Kwa mujibu wa ripoti zilizopatikana, Sheffield United ipo kwenye mazungumzo na Man United kwa ajili ya kunasa saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

Pellistri amekuwa akihusishwa sana kuondoka Man United kwa mkopo kwenye dirisha hili, licha ya kwamba aliingia akitokea benchi kwenye mechi zote mbili za Ligi Kuu England ilizocheza miamba hiyo ya Old Trafford msimu huu.

Mashabiki wa Man United hawafurahishwi na wazo la mchezaji huyo kuondoka, ambapo shabiki mmoja aliandika kwenye Twitter: “Anayepaswa kuondoka ni Antony.”

Shabiki mwingine aliongeza: “Ndiye winga wao bora kwa sasa, wasifanye hii kitu.”

Shabiki wa tatu aliandika: “Anayepaswa kuondoka kwa mkopo ni Antony”

Na shabiki mwingine alindika: “Mpelekeni Antony badala yake.”

Pellestri aliwakosha sana mashabiki kwenye mechi za Pre-Season, ambapo wengi walimpigia debe apewe muda wa kutosha wa kucheza.

Baba Msuva apangua usajili Simba, Young Africans

Tangu alipoanza kucheza mechi yake ya kwanza kwenye kikosi cha Man United, Januari mwaka huu, staa huyo ametumika kwenye mechi 12 za mashindano kwenye timu hiyo.

Amekuwa hapewi nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na Antony kucheza kwenye wingi hiyo ya kulia.

Antony ameanzishwa kwenye mechi zote mbili za ligi illizocheza Man United msimu huu, hajafunga wala kuasisti.

Na Mbrazili huyo tangu alipotua akitoka Ajax, amefunga mabao manane na kuasisti matatu katika mechi 46.

TPLB yafunguka ombi la Simba SC
Baba Msuva apangua usajili Simba, Young Africans