Kundi la mashabiki wa klabu ya Arsenal maarufu kama Arsenal Supporters Team (AST) limepiga kura ya kukosa imani na kocha, Arsene Wenger na maamuzi ya kura hiyo yakiwa ni kocha huyo Mfaransa aachie ngazi mwisho wa msimu huu.

Imeelezwa kuwa asilimia 88 ya wanachama wa kundi hilo jana wamepiga kura na kuadhimia katika kikao kuwa watawasilisha maoni yao kwa uongozi wa klabu hiyo ili ikiwezekana maonai yao yafanyiwe kazi ili mwisho wa msimu kocha huyo aachie ngazi.

Aidha, uamzi huo wa kupiga kura kwa mashabiki hao umekuja katika kipindi ambacho Arenal imepoteza mechi nne mfululizo katika mashindano matatu tofauti hali inayowafanya waamini kuwa uwezo wa mzee Wenger mwenye miaka 68 umefika mwisho.

Arsenal ilipoteza 2-1 mechi ya Europa League dhidi ya Ostersunds, kabla ya kufungwa na Manchester City 3-0 kwenye mchezo wa fainali ya kombe la ligi, na baadae kufungwa tena na vinara hao wa ligi kwenye mchezo wa ligi kuu kabla ya Jumapili kufungwa 2-1 na Brighton na Hove Albion kwenye mchezo wa ligi.

Hata hivyo, Katika kura hizo ambazo asilimia 88 wamesema Wenger aondoke mwisho wa msimu lakini silimia saba ya wanachama wamepiga kura ya Wenger kubaki huku asilimia tano kura zao zikiharibika.

 

Video: Musiba anatumika vibaya, siwezi kupuuza maneno yake- Yericko Nyerere
Township Rollers yaibutua Young Africans Taifa