Mashabiki wa Coastal Union ya Tanga leo wameendeleza vitendo visivyokubalika kwenye ulimwengu wa soka kwa kumpiga kama mwizi mwamuzi wa mchezo kati ya timu hiyo na KMC FC ya Dar es Salaam.

Mashabiki hao walioonesha kutoridhishwa na kichapo cha 3-2 nyumbani kwao kutoka kwa KMC FC, walivamia uwanja na kumshambulia mwamuzi Thomas Mkombozi kutoka Kilimanjaro.

Mwamuzi huyo alijikuta akiloa kipigo mbele ya askari polisi mmoja aliyekuwa uwanjani hapo ambaye alijitahidi kumsaidia bila mafanikio, hadi nguvu ya jeshi la polisi ilipoongezwa baadae.

Muuaji wa Coastal Union kwenye mechi hiyo ni mshambuliajni Joseph John wa KMC FC aliyeipachikia timu yake magoli mawili katika dakika ya 2 na ya 83 na goli lingine kuongezwa na Rashidi Roshwa kwa mkwaju wa penati dakika ya 89.

Mkwaju huo wa penati huenda ndio chanzo kikubwa cha mashabiki hao kuvunja amri za michezo na kumshambulia mwamuzi.

Magoli mawili ya Costal Union yalipachikwa na Bakari Nembo na Seif Mkenza katika dakika ya 52 na 72.

Walimu watoa siku 15 kwa Serikali kumaliza madai yao, ‘hatutaki lawama’
CUF walia na Polisi, wadai kuna ajenda ya siri dhidi yao