Baada ya matokeo ya bila kufungana dhidi ya Sporting Gijon, mkuu wa benchi la ufundi la Real Madrid, Rafael Benitez, amewataka radhi mashabiki wa klabu hiyo.

Benitez, alilazimika kufanya hivyo baada ya mashabiki wa The Galacticos kuonyesha hasira kufuatia matokeo hayo ambayo yaliwafanya kuondoka kwenye uwanja wa ugenini wakiwa na point moja.

Kabla ya kuomba radhi kupitia waandishi wa habari, Benitez alianza kuonekana akiwatuliza mashabiki wa Real Madrid kwa ishara.

Matokeo hayo yanatoa picha ya ushindani ambao unatarajia kuwepo kwa msimu huu, baada ya mambo kuwa magumu msimu uliopita kwa Real Madrid katika dakika ya lala salama.

Ushindi walioupata wapinzani wa Real Madrid katika mbio za ubingwa Atletico Madrid pamoja na FC Barcelona katika michezo yao ya ufunguzi wa ligi mwishoni mwa juma lililopita, ulikua chachu ya kuleta hasira miongoni mwa mashabiki wa Real Madrid ambao wameanza kuhisi huenda safari ya kuwakimbiza wapinznai wao ikawa ngumu.

FC Barcelona wao walifungua msimu wa ligi ya nchini Hispania kwa ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Athletics Bilbao, huku Atletico Madrid wakichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Las Palmas.

Lowassa, Duni Haji Wamshitaki Mkapa Kwa Wananchi
Rashid Saadallah Kuhojiwa Na kamati Ya Maadili