Hali ya utata imezidi kutanda kuhusu mashambulizi yaliyokuwa  wakifanyiwa maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kapenguria, kaskazini magharibi mwa Kenya.

Mshambuliaji huyo amekabiliana na maafisa wa polisi kwa takribani saa sita huku ikitajwa kuwa maafisa kadhaa wa polisi wameuawa.

Mkuu wa polisi Joseph Boinnet amesema mshukiwa huyo aliyekuwa amekamatwa na kuzuiliwa alimpokonya silaha afisa wa polisi na kuwafyatulia risasi askari waliokuwa zamu ya kulinda majira ya saa kumi na moja alfajiri.

“Juhudi zake za kutaka kutoroka zilizimwa na maafisa wengine waliofika mapema na kuzingira kituo, pia tumeagiza askari kuokoa mahabusu waliopo rumande- Boinnet.

Gazeti la Daily Nation la Kenya limemnukuu Kamishna wa Jimbo la Pokot Magharibi Wilson Wanyanga akisema mkuu wa polisi wa kituo hicho ni miongoni mwa maafisa waliouawa.

Taarifa za awali kutoka vyombo vya habari Kenya  zilisema kwamba shambulio hilo lilitekelezwa na watu waliotaka kumuokoa mshukiwa aliyekuwa amekamatwa.

Baadaye, polisi walisema ni mshukiwa mwenyewe aliyempokonya afisa wa polisi risasi na akawafyatulia risasi polisi akijaribu kutoroka, mshambuliaji aliripotiwa kupigwa risasi baadaye adhuhuri.

Mshukiwa huyo  ametambuliwa kama Omar Okwaki Eumod ambaye taarifa zinasema alikuwa amepangiwa kufikishwa Mahakamani Alhamisi asubuhi ya leo.

 

Video: Waziri Possi Ataka Watu Wenye Ulemavu kupewa kipaumbele
Afande Sele amzungumzia Mrithi wa 'Ufalme wa Rhymes', awabeza marapa