Ikiwa ni siku chache baada ya kuahirishwa kwa maandamano ya upinzani nchini Kenya, Kiongozi wa azimio la Umoja kwanza, Raila Odinga ametoa masharti mapya ya mazungumzo na Serikali, akitakata yasichukue zaidi ya siku 30.

Kiongozi huyo, alisisitiza upande wao kutokuwa na nia yoyote ya kupewa nafasi za uongozi katika Serikali iliyopo madarakani na kwamba kilio chao ni juu ya maisha magumu wanayoyapitia Wakenya hasa kupanda kwa gharama za maisha.

Amesema, “tumewaelekeza wajumbe wetu wawe wazi kwamba hatuwezi kuendelea na mazungumzo haya kwa zaidi ya siku 30 tangu yatakapoaanza,” alisema mwakilishi wa Odinga, Eugene Wamalwa kupitia taarifa yake.

Moja ya Maandamano yaliyowahi kufanyika jijini Nairobi. Picha ya Thomas Mukoya.

Aidha, muungano huo pia unataka serikali kuwaachia huru bila masharti vijana wanaoegemea mrengo huo ambao walikamatwa wakati wa maandamano ya awali wakidai hawakuwa na lengo baya isipokuwa kujaribu kupaza sauti kutafuta haki.

Azimio la Umoja huo, linasema wafuasi wake walikamatwa na kufikishwa mahakamani wakikabiliwa na kesi za kugushi wakiwatuhumu maofisa wa Polisi kwa kuwazuia lichaya wao kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama kwamba watafanya maandamano.

Masau Bwire: Ruvu Shooting tunamuachia Mungu
Arsena Wenger: Arsenal inanipa mashaka