Viongozi wawili kati ya 36 wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya ugaidi kwenye kesi ya jinai Na. 121/ katika Mahakama kuu ya Tanzania wameachiwa huru

Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu amesema kuwa amewafutia mashtaka viongozi wote wa jumuiya hiyo na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.

Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali Mselem walikuwa mahabusu tangu mwaka 2014 pamoja na wenzao kutokana na kukabiliwa na mashtaka hayo ambayo hayana dhamana wameachiwa huru Juni 15, 2021 baada ya DPP kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

“ni kweli wameachiwa huru. Nimewafutia wote mashtaka yaliyokuwa yanawakabili. Sasa suala la kutoka gerezani kama wameshatoka wote au wangapi hilo ni suala la taratibu za Magereza lakini mimi nimewafutia mashtaka wote.” Amesema Mwakitalu

Washtakiwa hao walikuwa wanadaiwa kujihusisha na makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 27(c) cha sheria ya kuzuia ugaidi ya 2002 Januari 2013 na Juni 2014.

Jay- Z amfikisha Mahakamani mpiga picha wake
Makala: Kwanini leo ni siku ya Mtoto wa Afrika?