Mashindano ya kumsaka Miss East Africa 2021, yanatarajia kufanyika  Novemba, mwaka huu, jijini Dar es Salaam na kushirikisha nchi 15 ambapo yatatoa nzuri ya kwa Tanzania kujitangaza kupitia utalii na uwekezaji.

Makamu wa Rais wa mashindano hayo Jolly Mutesi ambapo amesema kuwa mashindano hayo yameandaliwa na Rena Events Limited ya mkoani Dar es Salaam.

Mutesi ambaye yupo nchini kwa ziara wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya awali amesema mashindano hayo ni makubwa ya urembo kwa ukanda wa Afrika Mashariki yakitarajiwa kuangaliwa na watu wengi zaidi duniani.

Aidha amesema, mashindano hayo yatarushwa mubashara kupitia televisheni, ametaja nchi ambazo zitashiriki kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Tanzania Somalia, Madagascar, Malawi, Ushelisheli, Sudan Kusini, Comoro na Mauritius.

Mashindano hayo yalibuniwa na kuanzishwa na Rena Callist yalianza mwaka 1996 na kuwahi kufanyika Burundi kwa udhamini wa Hayati Rais Piere Nkurunzinza.

“Kuanzia sasa mashindano ya Miss East Africa yatakuwa yakifanyika kila mwaka, yatasaidia katika kudumisha umoja wa Afrika Mashariki, kukuza utalii, kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji,” amesema Mutesi.

“Mashindano pia yatatoa elimu na kusaidia katika changamoto mbalimbali hasa zinazowakabili wanawake na watoto wa ukanda huu wa Afrika ya Mashariki.

Aidha ametoa wito kwa makampuni mbalimbali yanayohitaji kutangaza biashara zao ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kupitia mashindano hayo.

Maafisa wanaotoa chanjo wauawa katika nchi isiyoamini chanjo
Mkutano wa NATO wamalizika, China, Urusi zakemewa