Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameyataka mashirika ya umma kujitafakari na hatimaye kurejea utaratibu wa kuuza hisa kwa wananchi, ili kuwapa umuliki.
Rais Samia ameyasema hayo akiwa jijini Arusha, wakati alipokuwa akifungua Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kinachofanyika leo katika Ukumbi wa AICC.
Amesema, “Mashirika yakajitafakari na yale ambayo yanaweza kurudi sokoni kwa wananchi na kuuza hisa zake ziuze ili wananchi wawe na umiliki.”
“Nataka Watanzania warejee kwenye utaratibu wa kununua hisa za mashirika yetu ya umma kama ilivyokuwa zamani. Kwa sasa wapo wananchi wenye uwezo wa kununua hisa hata kama ni kidogo kidogo,” amesisitiza Rais Samia.