Mashujaa FC kutoka mkoani Kigoma wanazidi kujiimarisha ikiwa ni msimu wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.

Timu hiyo itashiriki Ligi Kuu baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa mtoano dhidi ya Mbeya City ambayo itashiriki Championship msimu ujao 2023/24.

Katika usajili wao walikamilisha mapema dili la mtaalamu wa mapigo huru kiungo Ismail Mhesa aliyekuwa anakipiga ndani ya Mtibwa Sugar wamemuongeza mtaalamu mwingine.

Ni kiungo Hassan Hadji Cheda kutoka aliyekuwa anakipiga ndani ya Zimamoto anaingia kwenye orodha ya nyota wapya ndani ya Mashujaa FC ya Kigoma

Timu hiyo imeweka kambi Zanzibar kwa maandalizi ya msimu wake mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ipo chini ya Kocha Mkuu Mohamed Abdallah, ‘Bares’.

Bares ameweka wazi kuwa, wanaendelea na maandalizi kwa umakini ili wapate matokeo kwenye mashindano watakayoshiriki.

“Tupo kwa ajili ya maandalizi na tunatambua ushindani utakuwa mkubwa hivyo tupo tayari na wachezaji wanajituma,” amesema.

Jezi zenye Kamera zaibua mvutano EPL
Chelsea imekwama tena kwa Moises Caicedo