Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu msanii wa filamu nchini, Agnes Gerald maarufu kama Masogange, kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Shilingi 1.5 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili.

Mahakama imemuhukumu kosa la kwanza likiwa ni kutumia dawa za kulevya aina ya heroine, na la pili likiwa ni kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

Masogange alikamatwa na Polisi baadae, Jeshi la polisi lilikabidhi sampuli kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuthibitisha kama mlimbwende huyo anatumia dawa za kulevya.

Aidha mnamo Februari 22, mwaka jana, Agnes Masogange alifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam na kupitia sakata hilo mlimbwende huyo aliachiwa huru kwa dhamana ya Milioni 10 na wadhamini wawili, na shauri hilo lilisomwa tena tar 21 March kutokana na upelelezi kutokamilika.

Masogange ni miongoni mwa watu maarufu nchini, waliohusishwa na sakata la matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya, katika vita kali iliyoanzishwa na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mnamo Februari, 2017.

 

 

 

Magufuli amkubali Goodluck Gozbert kwa ....''Hawawezi kushindana''
Mtulia, Dkt. Mollel wala kiapo Bungeni