Mshambuliaji kutoka England Mason Greenwood ameendelea kukiwasha kwenye Ligi Kuu ya Soka nchini Hispania ‘La Liga’ na juzi Jumatano (Septemba 27) usiku allanza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha kwanza cha Getafe na kutoa asisti ya bao.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United anayekipiga huko kwa mkopo wa msimu mzima alipangwa katika kikosi cha kwanza kilichocheza dhidi ya Athletic Bilhao.
Wageni wa mchezo huo, Getafe walijikuta wapo nyuma kwa bao 1-0 katika dakika ya sita tu ya mtanange huo kabla ya Gason Alvarez kusawazisha kati ka dakika ya 51 baada ya Greenwood kumwekea pasi ya bao.
Hata hivyo, nyota wa kimataifa wa Hispania, Inaki Williams aliinyamnazisha Getafe na kufunga bao katika dakika ya 62 ya mchezo huo wa La Liga.
Getafe ilipambana na kupata Sare ya mabao 2-2 katika dakika va 83 baada ya Juanmi Latasa kufunga bao zikiwa zimabaki dakika saba.
Greenwood mwenye umri wa miaka 21, alijiunga na Getafe kwa mkopo wa msimu mzima dakika chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Alicheza mechi yake ya kwanza akitokea benchi dhidi ya Osasuna na akasaidia Getafe katika ushindi wa mabao 3-2.
Katika mchezo huo mashabiki wa Osasuna walimdhihaki Greenwood, hata hivyo kocha wa timu hiyo Jagoba Arrasate alimtetea na kukemea vitendo hivyo.
Greenwood pia alitokea benchi kwenye mechi nyingine ya La Liga dhidi ya Real Sociedad mwishoni mwa juma lililopita iliyopita ambayo ilipokea kichapo cha mabao 4-3.
Mara ya mwisho Greenwood kuichezea Man United ilikua dhidi ya West Ham kwenye mechi ya Ligi Kuu England Januari mwaka 2023.