Klabu ya Manchester United imefanya mazungumzo na Atalanta ya Italia kuhusu uwezekano wa kumnunua Mason Greenwood kwa mkopo, kwa mujibu wa 90min.

Greenwood alisimamishwa Man United tangu Januari 30, 2022, baada ya kushtakiwa kwa jaribio la ubakaji.

Mashtaka dhidi ya Greenwood yalitupiliwa mbali na mahakama Februari, lakini mchezaji huyo alibakia kusimamishwa na United kwa kipindi kilichosalia cha msimu uliopita, huku klabu hiyo ikifanya uchunguzi wa ndani.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ana mkataba na United hadi Juni 2025 huku klabu ikiwa na chaguo la kuongeza mkataba huo kwa mwaka mmoja.

United imekuwa ikifikiria jinsi ya kuendelea na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 na wamefanya mazungumzo na Atalanta juu ya uwezekano wa kumpeleka mchezaji huyo kwa mkopo kule Serie A.

Mazungumzo yamefanyika kuhusu uwezekano wa United kununua Hojlund huku Greenwood ikipelekwa kwa mkopo Bergamo kwa kubadilishana, ingawa inaeleweka kuwa Atletico Madrid nao wanamtaka Greenwood pamoja na Borussia Dortmund.

Greenwood amepigwa picha akifanya mazoezi peke yake wiki za hivi karibuni na hajarejea United kwa ajili ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya.

Kouassi Atohoula kumbadili Djuma Shaban
Wengine watatu kutambulishwa Simba SC