Mambo yamezidi kumwendea hovyo kinda wa Manchester United, Mason Greenwood kwani bado hajapata timu ya kuchezea ndani ya Ligi Kuu England, kwa hiyo atalazimika kwenda nje ya nchi akasake maisha mapya.

Klabu chache ndani ya ligi hiyo zilionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 lakini imeonekana kwamba zinaogopa kutokana skendo yake iliyomkabili.

Ilidhaniwa kwamba Greenwood angerudi Old Trafford kuendelea na majukumu yake lakini uongozi wa Man United ukaamua kumtema licha ya kesi yake kufutwa mahakamani.

Gazeti la Sun limeripoti kwamba Besiktas kutoka Uturuki ni moja ya timu mbili zinazomtaka Mshambuliaji huyo mwenye uwezo kufunga mabao makali.

Hata hivyo, hakuna sababu ya kuharakisha dili la kumsajili hata kama dirisha la usajili la England litafungwa rasmi leo kwani timu za Uturuki zitaendelea na ishu za usajili hadi Septemba 25 na pia kwa kuwa mchezaji huru anaweza kusajiliwa wakati wowote.

Endapo Man United itashindwa kumtafutia timu ya kucheza klabu hiyo itamlipa mkataba wake wa Pauni 75,000 kwa wiki ambao ndio mshahara wake.

Hata hivyo, bado atakuwa amebakiza mkataba wa miaka miwili kukiwa na chaguo la kuongeza mkataba mwingine wa miezi 12. Hiyo inamaanisha kwamba Greenwood atalipwa Pauni 8 milioni.

Kabla ya kutemwa, Greenwood aliamini kwamba angerudi Man United na alionekana akiwa bize akipiga matizi ya kufa mtu kabla ya msimu kuanza, lakini alisikitishwa baada ya klabu yake ya tangu utotoni ilipomtema.

Greenwood alisimamishwa tangu Januari mwaka jana kwa tuhuma za kutishia kuua na kubaka lakini mashtaka yake yalifutwa.

Skudu aenguliwa Young Africans
Erick Johora: Sikutarajia kuitwa Taifa Stars