Meneja wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC Massimiliano Allegri, ameendelea kusumbuliwa na tetesi za kuihama klabu hiyo, na kutimkia kaskazini mwa jijini London mwishoni mwa msimu huu.

Allegri, anatajwa kuwa katika mpango wa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger ambaye huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu, pindi mkataba wake utakapomalizika.

Meneja huyo amekua akisumbuliwa na vyombo vya habari kuhusu tetesi hizo, na mara kadhaa amezijibu kwa kukanusha uvumi huo, ambao ulianza baada ya kuonekana jijini London mwanzoni mwa mwezi uliopita.

“Bado nina mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuifundisha Juventus FC, nipo vizuri na wala sitetereshwi na tetesi za kuhamia Arsenal mwishoni mwa msimu huu,” Amesema Allegri.

“Nipo mbioni kuondoka? Tunapaswa kufikiria kwanza kabla ya kuuliza, kwa sasa nipo kwenye mpango wa kuisaidia Juventus ili iendelee kufanya vizuri katika ligi ya Italia na Ulaya. Ninapaswa kupewa muda wa kufanya mambo haya na sio kuingizwa katika tetesi ambazo hazina faida kwangu wala kwa muajiri wangu.

“Ninaomba tuwe watulivu na ukweli utafahamika  mwezi Juni, kama nitaondoka ama ninaendelea kubaki.” Alisisitiza Allegri.

Majaliwa: Rais hajatangaza kufuta vyama vya upinzani
Zanzibar kuwa makao makuu ya kiswahili