Kwa mujibu wa kampuni ya mitandao ya kijamii ya Hopper Hq imetoa ripoti ya watu maarufu duniani wanaoongoza kwa kuinguza mkwanja mrefu zaidi kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.

Ambapo ripoti hiyo imewataja watu maarufu wanaojishughulisha kucheza mpira wa miguu wanaongoza kwa kuingiza pesa ndefu zaidi kupitia mtandao wa Instagram kama vile.

Imemtaja Cristian Ronaldo, Lionell Messi, Neymar, David Beckham,  wengine ni Kendrall Jenner ambae ni mwanamitindo mkubwa nchini Marekani na Selena Gomez mwanamuziki maarufu Marekani amewahi kutoka kimapenzi na msanii Justin Beiber, mahusiano yao yalikuwa ni moja ya mahusiano pendwa na maarufu zaidi duniani kote.

Cristian Ronaldo anatajwa kuwa ndiyo  na mtu maarufu zaidi duniani na wa kwanza anayeingiza pesa ndefu kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo yeye anaingiza dola za Kimarekani milioni 47.8 kiwango ambacho kinatokana na matangazo anayoweka katika ukurasa wake, pia pesa hiyo inatajwa kuwa ni zaidi ya mshahara anaolipwa Juventus.

Hadi sasa Cristian Ronaldo anazaidi ya wafuasi milioni 186.

Akifuatiwa na Lionel Messi yeye anaingiza dola za kimarekani 23.3 milion, yeye anashika nafasi ya pili kwenye listi ya watu maarufu wanaoingiza mkwanja mrefu kupitia Instagram, anawafuasi  milioni 133 idadi hiyo ya wafuasi ni sawa na idadi ya wafuasi wa instagram wa msanii wa muziki mkubwa zaidi duniani ambaye anashika nafasi ya pili kwa kuwa mrembo wa dunia, Beyonce Knowless ambaye naye anawafuasi milioni 133 lakini hajaingia kwenye rekodi ya watu maarufu wanaolipwa mkwanja mrefu kupitia kurasa zao za Instagram hii ni kwa sababu wacheza mpira wengi wanafuatiliwa zaidi duniani kote.

Kendal Jenner mwanamitindo na mtangazaji wa vipindi vya runinga kutoka familia ya kitajiri ya Kriss Jenner na Catitlyn Jenner yeye alizaliwa 1995 ni moja ya vijana wadogo ambaye anashikilia nafasi ya 3 kwa watu maarufu wanaoingiza pesa ndefu kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo rekodi yake inaonyesha Kendrall  anaingiza dola za kimarekani 15.9 milioni, na sasa anawafuasi milioni 117 kupitia ukurasa wake wa instagram.

Aidha, watu wengine maarufu wanalipwa vizuri na mtandao wa Instagram ni David Beckam ambaye anaingiza dola za kimarekani 10.7milioni, Selena Gomez $8 milioni na Neymar $7.2 milioni.

 

 

Dar yaibuka kinara uandikishaji wapiga kura
Majaliwa aagiza kuta zibomolewe Hospitali ya Wilaya Ruangwa