Umoja wa Mataifa – UN, umeonya kuwa watu bilioni moja katika mataifa 43 duniani wapo katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu.
Hadi sasa nchi 24 zimeripoti mripuko wa kipindipindu ikilinganishwa na mataifa 15 yaliyoripoti hilo mwezi Machi mwaka jana.
Hatari ya mripuko huo inasababishwa na ongezeko la umasikini, migogoro, mabadiliko ya tabia nchi pamoja na watu kukosa makazi yao kufuatia sababu hizo.