Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula Von Der Leyen ameyahimiza mataifa yaliyo katika umoja huo kujenga muungano imara wa afya, akiahidi kuunda wakala wa utafiti wa tiba ya kibayolojia na kuandaa mkutano wa kimataifa.

Von der Leyen amesema janga la virusi vya corona limetilia mkazo haja ya ushirikiano wa karibu zaidi, akisisitiza kwamba watu wanaendelea kuteseka.

Amesema atashirikiana na Italia wakati itakapochukua nafasi ya urais wa kupokezana wa kundi la mataifa 20 yaliyostawi zaidi duniani G20, kuitisha mkutano wa kilele wa afya wa viongozi wa dunia mwakani, ili kushirikishana mafunzo ya mzozo wa virusi vya corona.

Aidha ameyaonya mataifa kutochukua hatua kwa ubinafsi litakapokuja suala la chanjo, ambayo inatazamwa na wengi kama suluhuhisho la kukomesha mzozo wa janga la corona.

Rais wa PSG afikisha mahakamani
Jeshi la zimamoto nchini kukagua shule zote