Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ametaja janga la Uviko-19 lililoota mizizi Duniani, vita nchini Ukraine na janga la tabianchi kuwa yamevuka mipaka na kufanya dhima ya Umoja wa Mataifa kuwa muhimu zaidi kuliko wakati wowote.

Guterres, ameyasema hayo jijini Geneva wakati akiongea na vyombo vya Habari, na kudjanga la Corona limeota mizizi na kuongeza kuwa, chini ya asilimia 20 ya wakazi wa nchi za kipato cha chini wakiwa ndio pekee waliopata chanjo huku suala la kujikwamua kutoka janga hilo likiwa bado halina usawa.

Amesema, ili kupunguza umaskini, kukabili mabadiliko ya tabianchi, kuchochea nishati bora, marekebisho ya kidijitali na mifumo ya chakula, ni muhimu kuzingatia shirikiano wa kimataifa na mshikamano wa wadau kama ambavyo ripoti ya mwaka 2021 inavyoelekeza.

Athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi. Picha na UN.

Kuhusu vita ya Ukraine, Guterres amesema vimesababisha machungu kwa mamilioni ya watu nchini humo na nje ya nchi, huku akipaza sauti kwa mataifa kuzingatia mapambano ya kukabiliana na madhara ya janga la tabianchi na ukosefu wa usawa uliodumu kwa muda mrefu.

Amesema, “Kwa pamoja katika mifumo ya Umoja wa Mataifa, tulitoa sera na majawabu, kusaidia kuunda mikakati na kupaza sauti za walio mstari wa mbele na wanaoenguliwa na UN ilihamasisha hatua za kupunguza ukosefu wa usawa, kuhamasisha rasilimali na kuchochea uwekezaji wa maendeleo endelevu.

Aidha amesema, anasisitiza utangulizi wa ripoti yake kuwa mwaka mzima wa 2021, Umoja wa Mataifa kama jukwaa la kusongesha uchechemezi wa kimataifa na ushirikiano, utasaidia hatua kadhaa za kufikia malengo ya kupunguza athari zaidi zinazoweza kuzuilika.

Bungeni: Serikali yakanusha Samaki kuhifadhiwa kwa dawa za maiti
Puttin apata 'kigugumizi' usaidizi wa china kwa Urusi