Usajili wa wa Jude Bellingham kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United na shughuli zao zote za usajili wa dirisha kubwa la majira ya joto umezingirwa na hali ya sintofahamu hadi sasa huku sakata la kuipiga bei klabu hiyo likiendelea.
Vyanzo vya habari vinasema kuwa Erik ten Hag Man Utd ipambane na majirani zao Man City na Real Madrid kumchukua nyota huyo wa Uingereza anayetarajiwa kuondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu.
Hata hivyo bado kuna ukakasi kuhusu dili la Bellingham kutua United kutokana na kutokuwa na uhakika juu ya nani ataimiliki klabu hiyo msimu ujao kwa kuwa kwa sasa inaripotiwa iko sokoni inauzwa.
Chanzo hicho kiliripoti Novemba mwaka jana kuwa kinaamini City wapo katika nafasi nzuri na hakuna kilichotokea labda kubadili msimamo huo.
Uhusiano kati yao na Dortmund ni mkubwa sana na ulisaidiwa na mkataba ambao ulimshusha Erling Haaland viunga vya Etihad majira ya joto na inadaiwa mazungumzo ya awali yamefanyika.
Liverpool sasa wamejiondoa kwenye vita na kuamua badala yake kutumia fedha walizo nazo katika ujenzi mpya wa klabu, badala ya kutumia pauni milioni 110 kufanya usajili wa kifahari kwa mchezaji mmoja.
United wanamtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye atavunja rekodi ya uhamisho Uingereza lakini hali ya Old Trafford imezingirwa na mchakato unaoendelea wa uuzwaji na uwekezaji wa klabu.
Kama ilivyoripotiwa Jumatano, zabuni ya tatu na ya mwisho imeombwa na Raine, benki ya Marekani inayosimamia mchakato wa wamiliki wa klabu ambayo ni familia ya Glazer.
Matajiri kadhaa wameweka mzigo mezani kama Sheikh Jassim Bin Hamad Al Thani wa Qatar na bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe.