Aliyekuwa Kiungo wa Klabu za Chelsea, na Manchester United, Nemanja Matic amemuonya Meneja kutoka nchini Argentina Mauricio Pochettino kwa kumueleza atakayokutana nayo, endapo atakubali kufanya kazi Stamford Bridge.

Pochettino anapewa nafasi kubwa ya kuajiriwa na Uongozi wa Chelsea mwishoni mwa msimu huu, ili aanze kazi ya kukinoa kikosi cha klabu hiyo mwanzoni mwa msimu ujao.

Matic aliitumikia Chelsea katika Michezo zaidi ya 100 kuanzia msimu wa 2014-2017 amesikitishwa jinsi Klabu hiyo inavyopitia kipindi kigumu kwa sasa, halia mbayo imemfanya kufunguka kwa anachokiona.

Juzi Jumanne (Mei 02) Chelsea ilipokea kichapo dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England iliyochezwa na kuendelea kujikita kwenye nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi hiyo.

“Nadhani Pochettino atahitaji muda zaidi, Chelsea ilisajili wachezaji wengi wenye vipaji, lakini siku za usoni namaanisha msimu ujao kuna kazi kubwa ya kukijenga kikosi unaposajili wachezaji sita au nane wote wanatarajia watacheza. Hapa ndipo matatizo yanapojitokeza,” amesema Matic

Matic anaamini wachezaji wote vijana waliosajiliwa na mmiliki wa The Blues kwa jumla ya kitita cha Pauni 600 milioni kama Enzo Fernandez, Mykhaylo Mudryk na Noni Madueke wataendelea kuimarika taratibu.

Wakati huohuo taarifa ziliripoti Pochettino ameripotiwa kupitisha mpango wa usajili wa mshambuliaji wa Bayern Munich, Sadio Mane ili atue Stamford Bridge dirisha lijalo la usajili.

Kwa mujibu wa Football Insider, Pochettino aliwapa ruhusa Chelsea kukamilisha usajili wa Mshambuliaji huyo kutoka nchini Senegal, ambaye amewahi kuzitumikia Klabu za Southampton na Liverpool zote za England.

Kiwango cha Pavard chaishtua FC Bayern Munich
Juma Mgunda: Tunaifuata Azam FC Mtwara