Baada ya hekaheka za muda mrefu za zoezi la kuhesabu kura usiku mzima, hatimaye Tume ya Uchaguzi imetangaza matokeo ya majimbo ya Kawe na Ubungo yaliyozua sintofahamu kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, Halima Mdee wa Chadema amefanikiwa kutetea kiti chake katika jimbo hilo kwa kupata kura 107, 989 dhidi ya mpinzani wake wa CCM, Kippi Warioba aliyepata kura 90,145.

Katika jimbo la Ubungo, mgombea ubunge wa Chadema, Saed Kubenea ametangazwa kuwa mshindi baada ya kupata kura 87,777 dhidi ya mpinzani wake mkuu wa CCM, Dk. Didas Masaburi aliyepata kura 59,640.

Wakazi wa Dar es Salaam pia wameyapata matokeo rasmi ya Tume katika jimbo la Kigamboni ambapo Mgombea wa CCM, Faustine Ndugulile ametangazwa kuwa mshindi na mbunge mteule wa jimbo hilo akimzidi mshindani wake mkuu, Lucy Magereli wa Chadema .

Mussa Zungu alitangazwa tena kuwa mbunge wa Ilala.

Kwa upande wa jimbo la Kibamba, bado hakuna taarifa rasmi lakini mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika ameendelea kujigamba kuwa ameshinda kwa kishindo.

Mkwasa Atangaza Kikosi Cha Taifa Stars
Chameleone Amng’ang’ania Rais Museven Uchaguzi Mkuu