Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), leo limetangaza matokeo ya kidato cha nne na kuorodhesha shule kumi za sekondari zilizofanya vizuri zaidi.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Charles Msonde ameeleza kuwa shule binafsi ndizo zilizoongoza kwa kufanya vizuri zaidi katika matokeo hayo.
Dkt. Msonde mezitaja shule kumi zilizopata ufaulu wa juu zaidi zilizokuwa na watahiniwa kuanzia 40 na kuendelea kuwa ni:
- St. Francis Girls (Mbeya)
- Kemebos (Kagera),
- Marian Boys (Pwani)
- Marian Girls (Pwani),
- Ahmes (Pwani)
- Canossa (Dar es Salaam),
- Bright Future Girls (Dar es Salaam),
- Maua Seminary (Kilimanjaro),
- Precious Blood (Arusha)
- Bethel Sabs Girls (Iringa).
Kwa mujibu wa orodha hiyo, mwaka huu shule kadhaa ambazo zilikuwa miongoni mwa shule kumi bora katika mtihani ulioanyika 2017 zimetupwa nje ya ulingo huo. Shule hizo ni pamoja na Feza Boys (Dar es Salaam), Anwarite Girls (Kilimanjaro), Feza Girls (Dar es Salaam) na Shamsiye Boys (Dar es Salaam).
Aidha, Dkt. Msonge amemtaja Hope Mwaibanje aliyekuwa anasoma shule ya Sekondari ya IIboru iliyoko jijini Arusha kuwa ndiye mwanafunzi aliyefaulu vizuri zaidi Kitaifa.
Matokeo hayo ni ya mtihani uliofanyika katika robo ya mwisho ya mwaka 2018.